32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

SHAMBULIO LA SUMU LAUA 90 SYRIA

DAMASCUS, SYRIA


WAFANYAKAZI wa uokoaji pamoja na madaktari walioko eneo la Mashariki mwa Ghouta nchini Syria, wamethibitisha kuwa watu zaidi ya 90 wamefariki dunia katika shambulio baya la kemikali.

Serikali ya Rais Bashar Al- Asaad wa Syria imekanusha kutumia kemikali hiyo dhidi ya raia.

Mamlaka za usalama Marekani, zinasema zinafuatilia kwa karibu taarifa zinazohuzunisha za matumizi ya silaha za kemikali wilayani Ghouta Mashariki.

Kundi la White Helmets, ambalo ni la utoaji msaada, limechapisha picha za maiti nyingi kwenye mtandao wake wa kijamii, zikiwa ndani ya chumba kimoja cha ghorofa ya chini ya jumba moja, zikiwemo picha za wanawake na watoto waliofariki.

Hata hivyo, picha hizo bado hazijathibitishwa.

Awali, ilisemekana kuwa, watu 150 waliuawa, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.

Shambulio hilo linaloshukiwa kuwa la kigaidi, lililolenga mji wa Douma, eneo linaloshikiliwa na waasi Mashariki mwa mji wa Ghouta, limetokea baada ya majuma kadhaa ya mlolongo wa milipuko ya mabomu kutoka angani ya wanajeshi wa Syria.

Raia wapatao zaidi ya 100, wanasemekana kukwama huko, kwa pamoja na wapiganaji waasi.

Televisheni ya taifa la Syria, imelilaumu kundi kuu la waasi la Jaish al-Islam, kwa kutia chumvi juu ya shambulio hilo, katika jaribio la lililoshindwa la kuzuia juhudi za jeshi la Syria kuendelea mbele kuwakabili.

Kumekuwa na mashambulio kadhaa ya kemikali ambayo yametokea nchini Syria, katika mapigano hayo makali yaliyodumu kipindi cha miaka saba iliyopita.

Mashambulio hayo yamelaaniwa vikali na mataifa mbalimbali huku Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Duniani Papa Francis akisema ni njia za maangamizi zisizo na sababu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles