31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAKANUSHA TUHUMA ZA TUCTA

Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM

SERIKALI imekanusha tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Tuhuma hizo ni kupandisha mshahara, madaraja wafanyakazi, kushindwa kutimiza ahadi yake ya kushughulikia madai ya wafanyakazi na kuondoa kazini wafanyakazi wa darasa la saba ambao waliajiriwa kabla ya mwaka 2004.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, alisema Serikali tayari imeishaijibu kwa ushahidi wa video moja ya tuhuma hizo, hususan ile ya TUCTA kulaani kauli inayodaiwa kuwa ni ya Rais aliyoitoa kwenye mkutano wa ALAT, ambayo inadai kwamba, Rais hatapandisha mishahara ya watumishi wa umma, hoja ambayo ilipotoshwa pia na Chadema.

Katika kujibu tuhuma hiyo, Dk. Abassi alifafanua kwamba, Rais alijibu hoja mahususi ya posho za madiwani ambao walitaka kuongezewa kutoka Sh 350,000 hadi Sh 800,000, sawa na asilimia 150 na si vinginevyo.

Aliongeza kwamba, watu wanaoendelea kueneza uzushi kwamba Rais alisema kuwa hataongeza mshahara kwa watumishi wa umma waache, la sivyo watachukuliwa hatua.

“TUCTA wameendelea kuisemea Serikali kwamba kuna mambo ambayo hayajatekelezwa, ukiachia suala la ALAT, kuna hoja ya watumishi walioghushi vyeti na walioondolewa kazini ambao kimsingi ni wale wa darasa la saba kabla ya waraka wa 2004.

“Dai hilo halina msingi, kwa sababu ule waraka ulikuwa wazi kwamba, kuanzia 2004 kuja juu watumishi wote wanapaswa kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea, lakini kilichotokea kuna watu elimu yao ilikuwa darasa la saba baada ya waraka huo, wakaamua kufoji vyeti ili  waweza kupandishwa vyeo na mishahara.

“Kwa sababu msimamo wa Serikali kwa nini walighushi vyeti, kwa hiyo hawakuwa na sifa za kuendelea kuwapo katika utumishi na sehemu ya walioondolewa na kama yupo ambaye amesimamishwa aliajiriwa kabla ya 2004 atuletee ushahidi tutaufanyia kazi,” alisema Dk. Abassi.

Kuhusu madai ya kutopandishwa madaraja kwa watumishi, Dk. Abassi alisema madai hayo Rais mwenyewe akiwa kwenye sherehe za Mei Mosi aliyajibu kwamba, asingepandisha wakati mchakato wa uhakiki wa wafanyakazi hewa unaendelea na kuahidi utakapomalizika wote wenye haki yao wataipata.

Kuhusu tuhuma za kwamba serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kushughulikia madai ya wafanyakazi, Dk. Abassi alisema Serikali inaendelea kuyashugulikia madai ya watumishi wote.

Kwa mtazamo huo, Dk. Abassi alivitaka vyama mbalimbali vya wafanyakazi na vyama vya siasa kufanya mambo yao kisayansi, pamoja na kwamba wana haki ya kuhoji, lakini wasikurupuke kuzungumza vitu ambavyo hawana uhakika.

“Tayari Serikali imeshatumia Sh bilioni 70 kulipa madai ya wafanyakazi ya mwaka 2016/17 na katika bajeti ya mwaka huu kuanzia Julai mpaka sasa imetumia Sh bilioni 37.4.

Pia alisema sheria ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016 inawafanya watumishi serikalini kutoa taarifa ambazo ziko wazi na asiyezitoa atachukuliwa hatua, hivyo kuvitaka vyama vyenye hadhi kama TUCTA kabla ya kutoa taarifa kuuliza kwanza kabla ya kulalamika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles