Na Shomari Binda, Musoma
Jumla ya Sekondari mpya tano zinatarajiwa kufunguliwa katika Jimbo la Musoma vijijini mkoa wa Mara ili kupunguza wingi wa wanafunzi madarasani na kutembea umbali mrefu.
Kukamilika kwa madarasa hayo kunatokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya nguvu za wananchi na mbunge wa jimbo hilo, Prof. Sospeter Muhongo.
Akizungumza na Mtanzania Digital Katibu wa mbunge huyo, Hamis Gamba amesema kukamilika kwa shule hizo kutafikisha jumla ya shule 27 za sekondari zikiwemo mbili za binafsi.
“Kata ya Lifulifu ni moja ya kata ambazo zilikuwa hazina shule ya sekondari na kwa sasa tunakamilisha shule hizo,” amesema Gamba.