24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Makete asota barabarani, Tanroad wajibu

Na Mwandishi Wetu, Makete

Kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha wilayani Makete, mawasiliano ya barabara ya Makete-kwenda Mbeya kupitia Ipelele yamekatika kwa muda sasa kitu kilichopeleka Mbunge wa Makete, Festo Sanga kufika eneo la tukio kusaidiana na wananchi kutatua kero hiyo.

Sanga aliyewasili mlima wa ipelele majira ya saa mbili asubuhi hii leo Desemba 28, amefika na kusaidia kutatua changamoto hiyo kwa kusaidiana na wananchi kukwamua gari ya wasafiri iliyokuwa inakwenda Mbeya.

Pamoja na jitihada hizo, mbunge huyo aliwasiliana na TANROAD Mkoa wa Njombea ambao kwa uharaka wamefika eneo la tukio na kesho Desemba 29, mkandarasi atakuwa eneo la kazi kuanzia asubuhi ili kuhakikisha changamoto hiyo inatibika ili wasafirishaji na wasafari waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Aidha, mbunge huyo amesisitiza, nia ya serikali ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ipo na tayari mkakati wa serikali kuanza ujenzi upo njiani unakuja, hivyo anawekeza nguvu zake kwa serikali kuikumbusha umuhimu wa barabara hiyo na zingine zinazoiunganisha Makete akitolea mfano Chimala-Matamba-Kitulo na ile ya Kipengele-Lupila.

“Makete inachangamoto kubwa ya barabara kutokana na mvua nyingi zinazo nyesha kwa muda mrefu na wakati huo huo magari makubwa ni mengi yanayoingia kupakia dhahabu ya Makete (Mbao, Viazi na matunda), hivyo uhitaji wa barabara ya lami ni mkubwa sanaa.

“Hivyo nami kama mbunge nitapambana kuhakikisha kuwa miundombinu yetu inakuwa imara kwa ajili ya wananchi wetu na uchumi wa Tanzania kwa ujumla,” amesema Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles