Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Bima ya Sanlam imezindua kauli mbiu mpya ya (Live with Confidence) yenye lengo la kuwafanya wateja wa kampuni hiyo na Watanzania kwa ujumla kujiamini wanapotuia huduma za kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Ijumaa Mei 7, 2021 jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam, Julias Magabe amesema kuwa kauli mbiu hiyo imebeba mwendelezo wa utoaji huduma bora kwa Watanzania.
“Leo ni siku nzuri kwangu kwani tunakwenda kuzindua kali mbiu na dhima nyetu mpya isemayo “Live with Confidence” yaani ishi kwa kujiamin. Hii siyo kauli mbiu mpya tu ya Sanlam au maneno mafupi yanayokaa chini ya nishani ya kampuni yetu kama tu utamaduni.
“Hapa hii ni ahadi yetu kwa wateja wetu na jamii nzima ya Watanzania, ni ahadi ya kufanya kila linalowezekana kwenye utoaji wa huduma zetu, kumfanya mteja wetu kuishi kwa kujiamini akiwa na Amani kuwa anayokinga madhubuti ya kifedha dhidi ya madhara yanayotokana na majanga mbalimbali ya kimaisha ama mani ya kuwa bima yake ya akiba itaiva na kumwezesha kutimiza malengo yake,” amesema Magabe.
Magabe amesema kuwa huduma ya bima zina umuhimu mkubwa kwa mstakabali wa taifa, uchumi wake na wanachi kwa ujumla, kwani kinga zinazotolewa na kampuni za bima, husaidia, mlaji wa huduma kujikinga na athari za kiuchumi zitokanazo na majanga mbalimbali ikiwemo moto, mafuriko, wizi, ajali, ulemavu na hata vifo.
“Kwetu Sanlam tunajivunia kuwa sehemu yay a utoaji wa kinga hii muhimu nchini Tanzania na kupitia bima zetu mbalimbali zitolewazo na SGI & SLI hulipa mafao ya bima yapatayo wastani wa Sh bilioni 40 kila mwaka,” amesema.