NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MSANII Ruby na kundi la Weusi, wameacha mjadala wa nguvu mjini Songea baada ya juzi kushusha burudani ya nguvu katika tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote, lililofanyika Uwanja wa Majimaji mkoani humo.
Kabla ya kuingia mkoani humo, tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro kabla ya kwenda mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea, wakati leo litatimua vumbi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, ambaye aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Pololite Mgema, ndiye aliyefungua tamasha hilo.
Mkuu huyo wa mkoa aliishukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kulipeleka tamasha hilo kubwa.
“Hii si kwa burudani pekee, bali ni fursa kwa wakazi wa mkoa huu kwa kuwa umewawezesha kuongezea kipato kipindi hiki chote cha wiki nzima.
“Niwapongeze tena Tigo na Clouds Media, nakuwaomba mwakani msiache kuja tena mkoa wetu,” alisema Christina.
Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumsaka mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota, ambapo msanii Single Baba aliibuka kidedea hivyo ataiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Shoo rasmi ilianza kwa msanii, Mesen Selekta, kufuatiwa na Rubby.
Rubby miaka kadhaa nyuma aliibuliwa kupitia shindano la Supa Nyota, aliteka hisia za mashabiki kupitia nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze, Ntade, Na Yule, Forever na nyingine.
Wasanii 12 walipanda jukwaani katika tamasha la Songea na kuwarusha vilivyo mashabiki wa muziki akiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid Q, Masen Selekta, Lulu Diva, Chege, Fobya.
Wasanii hao pia ndio watakaotoa burudani leo katika Uwanja wa Nangw’anda Sijaona, Mtwara.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, Kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Songea kufurahia promosheni zake katika msimu huu wa vibes. Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#.
Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa TigoPesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000, badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslimu.
Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Master pass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.
Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz nakuchagua Trivia.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu kwa asimilia 100 wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.