Saudia yakana kumdhuru Khashoggi

0
816

RIYAHD, SAUDI ARABIA


UTAWALA wa kifalme nchini Saudi Arabia, umetupilia mbali madai kwamba uliamuru kuuawa kwa mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi, kupitia kikosi maalumu ndani ya ubalozi wake mdogo wa mjini Istanbul nchini Uturuki.

Saudi Arabia imesema madai yaliyotolewa na Uturuki si ya kweli na hayana msingi, huku nchi hizo zikiwa bado zinavutana juu ya mkasa huo na hadi sasa hajulikani alipo.

Ujumbe wa Saudi Arabia ulikuwa nchini Uturuki kwa ajili ya mazungumzo juu ya kisa hicho cha Khashoggi ambacho kinatishia kuharibika uhusiano kati ya mataifa hayo mawili na pia kuharibu sifa ya mwanamageuzi Mwanamfalme Mohammed bin Salman pamoja na uhusiano wake na nchi za Magharibi.

Mzozo huo ukiwa unazidi kupamba moto, maofisa wa Uturuki wamesema kwamba kuna ushahidi uliorekodiwa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia unaothibitisha madai yao kwamba Khashoggi aliteswa na kuuliwa ndani ya jengo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here