TURIN, ITALIA
MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya taifa Ureni na klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kuwa, mipango yake na kuja kucheza filam mara baada ya kustaafu soka.
Nahodha huyo wa Ureno, amesema filamu ni moja kati ya vitu ambavyo anavipenda, hivyo haoni sababu ya kushindwa kufanya mara baada ya kutundika daruga.Ronaldo anataka kufuata nyayo za nyota wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona, ambaye kwa sasa anafurahia maisha yake mengine ya kucheza filamu mara baada ya kustaafu soka mwaka 1997 akiwa na klabu hiyo ya Man United.
Ronaldo itakuwa rahisi kuingia kwenye filamu kutokana na baadhi ya vitu ambavyo anavifanya na kumuingizia fedha nje ya soka kama vile kufanya matangazo mbalimbali ya mitindo na mambo mengine.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, bado hajamaliza kazi yake ya kucheza mpira na hadi sasa haijulikani lini atatangaza kustaafu soka kutokana na uwezo wake bado kuwa imara.
Akifanya mazungumzo na kipindi cha Dubai Sports Conference, mchezaji huyo alisema, “Muda ukifika wa kutangaza kustaafu soka nitarudi darasani kwa ajili ya kujifunza filamu. Akili yangu inawaza kusomea pamoja na kujifunza pia, baada ya kumaliza maisha yangu ya soka hakutokuwa na maswali tena kwa kuwa kila kitu kipo kichwani mwangu kwa sasa. Filamu ni kitu ambacho kinazunguka kwa sasa kwenye mawazo yangu,” alisema mchezaji huyo.
Hata hivyo, Ronaldo alisema hadi sasa hajui lini atatangaza kustaafu soka, ila anausikilizia mwili wake ufanya maamuzi ya kutaka kupumzika soka.
“Sijawahi kuwa na msimu mbaya katika maisha yangu tangu nimeanza kujitambua jinsi ya kupambana na changamoto. Nimekuwa nikishinda mara zote, lakini siku mwili wangu ukikataa kufanya kile akili inachokitaka nitatangaza kustaafu. Miaka ya nyuma wengi walikuwa wanastaafu wakiwa na miaka 30 au 32, lakini sasa hadi 40,”