30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia atoa msimamo kuhusu katiba mpya

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Katiba ya nchi siyo mali ya vyama vya siasa wala wanasiasa bali ni mali ya Watanzania awe na chama au hana, awe na dini au hana ni mali yake.

Dk. Samia ameyasema hayo leo Septemba 11, jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa Demokrasia unaolenga kutahimini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi na hali ya Siasa nchini unaofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNICC) uliokutanisha wadau mbalimbali wakiwamo Viongozi wa Dini, Wanahabari, Mabalozi, Asasi za Kirai na wadau wengine.

Amasema kila upande wa maoni ya Katiba Kikosi Kazi, Visiwani Zanzibar na wengine wote wanatoa kauli ni moja katiba mpya watakubaliana lakini jambo hilo ni mchakato.

“Hatuwezi amka tukakafanya marekebisho lete katiba ya Jaji Warioba(Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba) na nyingi weka hatuendi hivyo, hii ni mali ya Watanzania tukitak kufanya marekebisho lakini katiba ni kitabu tukatengeneza vizuri tukapamba takakiweka wangapi wanaelewa hicho kitabu yaliyomo ndani, wangapi wanaelewa?

“Unakwenda je kuchukua maoni Mtanzania kitabu hakijui tunaanza na elimu watanzania wajue katiba ni kitu gani, kinasema je, kina nini tunadhani viongozi wa kisiasa tuna right(haki) ya kuburuza watu? tunacho kisema sisi watu wote wafuate tunavyo sema sisi kila mmoja aongelee katiba hata wanavyosema wabadilishe katiba mpya ilete nini wanasema maendeleo hawajui,” amesema Dk. Samia.

Amesema kama kuheshimu vitabu wangeheshimu vya dini ndo vya kuheshimiwa huku akihoji ngapi hawaheshimu vitabu vya dini?.

Amesema huwezi kuheshimu Bibilia na Msaafu hadi wajue ndani kuna nini, hivyo katiba siyo kitabu ni morality na maadili yenye ubora yatakuwa hivyo kila mtu ajue na kuamini.

Amesema katiba inatakiwa iwekwe mioyoni mwa watu kila mtu ajiamini iwe itikadi yake katika nchi kama walivyofanya nchi nyingine na kwamba hawakurupuki.

“Ukienda vijijini ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wanajua katiba ninachohitaji kwa wanasiasa ni maoni katiba iwe je.

“Msajili wa Vyama vya Siasa nimemwambia nataka ushiriki wa maoni yao kwenye kamati naenda kuanzisha mchakato wa katiba nyinyi mtakuwa na wawakilishi huko kaeni mkubaliane vyama vingapi vitaingia siyo kila mtu ataingia, katiba siyo mali yetu tusivuruge wananchi,” amesema Dk. Samia.

Kuhusu Demokrasia

Akizumgumzia kuhusu Demokrasia nchini amesema inakwenda na nidhamu na njia ya kuendesha mambo ndani ya nchi mila, desturi, maadili na utamaduni

“Bara la Afrika kila nchi ina demokrasia tofauti, demokrasia utu wa mtu lazima uheshimiwa yale ambayo hutaki kufanyiwa basi usifanyie wenzio, demokrasi siyo matusi na demokrasia haina mfumo,” amesema Dk. Samia.

Rais Samia amesema kuwa tayari Serikali imeshaanza kutelekeleza mapendekezo ya kikosi kazi ikiwemo kuruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ambapo kwa sasa mikutano hiyo inafanyika sehemu mbalimbali nchini.

“Hatukutoa fursa ya mikutano ya hadhara ili watu kuvunja sheria, tumieni fursa hii kujenga Sera zenu kwa wananchi na si vinginevyo. Hakuna aliye juu ya sheria, atakaye fanya kosa atachukuliwa hatua za kisheria, kila mtu adumishe amani, umoja na mshikamano wa kitaifa”, ameeleza Rais Samia.

Ameongeza kuwa kuna uhuru wa kutoa maoni lakini una mipaka yake kisheria na kibinadamu na kuwa marekebisho ya Katiba yameanza kufanyiwa kazi, si mali ya vyama vya siasa bali ni mali ya Watanzania wote.

“Hatutakurupuka katika hili, tutaenda taratibu ili kuweka kila kitu sawa ikiwemo kutoa elimu kwa Watanzania ili kila mtu atoe maoni yake ya nini kibadilike, demokrasia sio matusi, demokrasia ni kutoa maoni, tusiitumie vibaya. Vyama vya Siasa nawakumbusha misingi yetu kufuatwa ambayo ni pamoja na kuheshimu maazimio yetu, kuheshimu sheria za Serikali, kuheshimiana”, amesisitiza Rais Samia.

Ameeleza kuwa Tanzania kuna misingi ya pekee ambayo wazee wetu waliisuka wakawambia hiyo ndio misingi wanakwenda nayo na yeyote anayeitakia mema nchi hii atakwenda kwenye misingi hiyo.

Awali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati akimkaribisha Rais Dk. Samia amesema kila Mtanzania anawajibu wa kutunza amani na umoja uliopo ili kuendeleza mshikamano.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenister Mhagama amesema mkutano huo wa siku tatu utafanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na vikosi kazi vyote viwili bara na visiwani pamoja na hali ya siasa nchini na kuangalia uchaguzi ujao.

Mapema, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alimuomba Dk. Samia kuendelea kufanya mikutano kama hiyo ili kufungua fursa zilizo minywa na kuweza kujadili changamoto na wadau wa siasa kupata matokeo chanya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nhini (TCD), Prof. Ibrahim Lipumba ameomba kufanywa mabadiliko katika baadhi ya vifungu vya katiba kuelekea uchaguzi mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles