24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi 13 za Kimataifa kuangazia hakimiliki za Ardhi jijini Arusha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi za Kimataifa kutoka mataifa 13 barani Afrika zinatarajia kukutana katika mkutano wa siku tatu utakaofanyika jijjni Arusha nchini Tanzania ukilenga kujadili utekeleza wa hakimiliki za ardhi kwa wenyeji wa Bara la Afrika baada ya tafiti kuonesha ongezeko la uelewa wa hakimilki za ardhi hususan kwa wenyeji wa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.

Kulingana na taarifa iliyotolewa leo Septemba 11, 2023 na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeeleza kuwa mkutano huo ni hatua muhimu ya kimkakati kuendeleza uwajibikaji na hatua zitakazopelekea utekelezaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira wa mwaka 2023 kwa lengo la kuimarisha utashi wa kisiasa, kukusanya rasilimali na kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa hakiardhi barani Afrika.

Mgeni rasmi wa Mkutano huu ni Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko: “Taasisi zitakazoshiriki katika Mkutano ni pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mawaziri wa kisekta kutoka nchi 13 za Afrika na utafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya jijini Arusha Septemba 12 hadi 14, mwaka huu.

“Serikali na Taasisi za Kimataifa barani Afrika zinaangazia usalama wa watu na jamii za jadi kama nyenzo muhimu ya amani ya jamii na maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika aidha, pamoja na juhudi hizi sheria na sera za zilizotungwa miaka 15 iliyopita bado hazijatekelezwa na kuna fursa chache miongoni mwa taasisi na taasisi na baadhi ya mataifa barani Afrika,” imeeleza taarifa hiyo ya Wizara ya Ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles