29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia atoa Bilioni 4 ujenzi wa soko la kisasa Nzega Parking

*Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh Bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la Nzega Parking lililoko wilayani Nzega mkoani Tabora ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dk. Samia ametoa fedha hizo mapema leo Jumatano Oktoba 18, 2023 alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko hilo.

Aidha, Rais Dk. Samia amewataka wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko hilo likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles