Mamilioni ya raia wa India wanapiga kura leo katika awamu ya tatu ya uchaguzi mkuu.
Zoezi hilo pia limefanywa na Waziri Mkuu Narendra Modi ambaye amepiga kura yake katika jimbo analotokea la Gujarat.
Modi kwa mara nyingine amesisitiza umuhimu wa kupambana na ugaidi akisema kuwa kitambulisho cha kura ndio silaha ya demokrasia.
Kwa ujumla, raia milioni 188 nchini India wamesajiliwa kupiga kura katika maeneo 177, ya majimbo 15 na mipaka inayodhibitiwa na serikali. Bunge la India lina wajumbe 545.
Tume ya uchaguzi imesema kufikia leo mchana, asilimia 24 ya watu walikuwa tayari wamepiga kura.
Mpaka sasa, chama tawala cha Bharatiya Janata – BJP kimeipigia debe rekodi ya Modi kuhusu usalama wa taifa wakati kikilenga kukabiliana na madai ya upinzani ya usimamizi mbaya wa uchumi, uhaba wa nafasi za kazi na matatizo ya wakulima.