28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Promosheni ya Jipate na Infinix yazinduliwa rasmi

*Wateja kukopeshwa bila ya riba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix imezindua rasmi promosheni ya ‘JIPATE NA INFINIX’ ikiwa ni mfumo ambao kampuni hiyo imejiwekea kila mwaka wanautumia mwezi Agosti kama mwezi wa Infinix ambapo kampuni hiyo inawafikia wateja wake kwa ukaribu zaidi kupitia ofa mbalimbali ikiwemo unafuu wa bei pamoja na kutoa zawadi kwa wateja lengo likiwa ni kutoa unafuu kwa kila mwenye kutamani kuishi kidigitali.

Balozi wa Promosheni hiyo Msanii, Frida Amani akizungumza leo Agosti 17, jijini Dar es Salaam: “Promosheni ya JIPATE NA INFINIX inafanyika kwa kipindi cha mwezi mzima jijini Dar es Salaam na mikoani ambapo ndani ya msimu huu mteja akinunua simu hizi za Infinix, Note 30, Note 30 pro, Note 30 vip, Zero ultra, Hot 30, Hot 30i, Hot 30 Play na Smart 7 utajiweka kwenye nafasi kupata Jokofu, pikipiki, Laptop na zawadi nyingine nyingi,” amesema Frida.

Aidha, ameongeza kuwa: “Nimekuwa mwanafamilia wa Infinix kwa muda mrefu tangu kipindi cha Infinix HOT 10T na hadi sasa nimekuwa nikivutiwa sana na simu za kampuni hii kikubwa kinachotofautisha simu za Infinix na zingine ni uhimili wa simu kukaa na chaji kwa muda mrefu simu za Infinix zipo imara sana ili kuthibitisha hili nunua Infinix mkoa wowote uliopo na jambo jema zaidi ukihitaji huduma ya kukopa ipo kwa simu zote za Infinix na Riba imeondolewa kabisa kwa Infinix NOTE 30,” amesema Msanii huyo.

Infinix Note 30 ilizinduliwa rasmi nchini Tanzania Juni mwaka huu ambayo ni simu yenye kuchaji kwa haraka ndani ya dakika 30 huku ikitoa asilimia 70 ya chaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles