Polisi nchini sudan imewaamuru maafisa wake kutowashambulia maelfu ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu wa jeshi mjini Khartoum tangu Ijumaa.
Waandamanaji hao wanamtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu.
Awali milio ya risasi ilisikika nje ya makao ya jeshi na ripoti zinasema kuwa maaskari wanaotoa ulinzi kwa waandamanaji wamepigwa risasi na maajenti wa serikali.
Katika taarifa yake Msemaji wa Polisi aliandika alisema wanatoa amri kwa vikosi vyote visiingilie maandamano ya amani au kuwashambulia wananchi.
“Tunamuomba Mungu asaidie kuleta utulivu nchini mwetu na kuwaunganisha Wasudan. na kufikiwa kwa makubaliano yatakayosaidia kupokezana madaraka kwa amani,” ilisema Msemaji wa Polisi
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo amesema waandamanaji saba waliuawa siku ya Jumatatu na wengine 15 kujeruhiwa, huku maafisa 42 wa vikosi vya usalama nao wakijeruhiwa pia.
Ameongeza kuwa karibu watu 2,500 wamekamtwa.