22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Wasanii kuwaburudisha polisi Kanda Maalum Aprili 10

BRIGHITER MASAKI

Wasanii wa tasnia ya muziki, filamu na wanenguaji Aprili 6 mwaka huu watatoa burudani katika sherehe ya kuwatunuku polisi Kanda maalum ya Dar es salaam.

Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Osterbay Jijini Dar es Salaam itafuatiwa na tafrija ya chakula cha usiku katika Ukumbi wa Mlimani City.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 10, mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere amesema wamejipanga kutoa burudani ya kutosha katika kuwapongeza makamanda hao wanao linda usalama wetu.

“Kila msanii atatoa burudani ya aina yake kulingana na tasnia ambayo yupo ili kuhakikisha tukio hili linafanikiwa, polisi wetu wanalinda amani na usalama wetu hivyo inabidi tuwapongeza,” amesema Steve.

Wasanii watakao shiriki siku hiyo ni Dude, Ketty, Irene Uwoya, Aunty Ezekiel pamoja na bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta.

Naye Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Lazzaro Mambosasa amesema sherehe hizo zitawajumuisha askari 70 wanaofanya kazi vizuri na wasio na vyeo.

“Kila mtu akifanya kazi vizuri anahitaji pongezi Ijumaaa tutatoa zawadi na tuzo kwa polisi wote wanaofanya kazi vizuri,”amesema Mambosasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles