24.6 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Picha ya kutisha ya faru yapata tuzo

Pretoria, Afrika Kusini

PICHA ya kutisha ya uhalifu wa mazingira, imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu.

Picha hiyo, iliopigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini, Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi ndani ya Hifadhi Hluhluwe Imfolozi.

Wawindaji haramu, walimuua mnyama huyo usiku kabla ya kumtoa pembe zake.

Stirton alipiga picha hiyo, ikiwa miongoni mwa uchunguzi kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru.

Mpiga picha huyo, alizuru zaidi ya maeneo 30 uliofanyika uhalifu huo, wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa kuogofya.

Stirton ambaye alipokea tuzo hiyo katika tamasha la chakula cha jioni lililofanyika jumba la kumbukumbu mjini London , anaamini  unyama huo aliofanyiwa faru  ulitekelezwa na wakazi wa eneo hilo.

Lengo kubwa la uwindaji huo,ni kuuza pembe mbili za faru huyo kwa wafanyibiashara.

Wafanyibiashara hao, baadaye huzipeleka pembe hizo hadi Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama Vietnam.

Katika mataifa hayo,pembe za faru zina thamani ya juu ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya Cocaine.

Biashara hiyo, hupata msukumo wa imani sawa na kucha za vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote kutoka saratani hadi mawe ya figo.

Brent Stirton aliambia BBC : Kwa mimi kushinda tuzo hii, kwa majaii kuweza kutambua kazi yangu ni wazi kwamba tunaishi katika muda tofauti na kwamba hili ni suala nyeti.

”Suala la kuangamia kwa baadhi ya wanyama ni la kweli na faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea kuangamia kwa kiwango kikubwa na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua picha yangu kwa kuwa inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine”.

Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la majaji hao wa WPY, alisema picha ya faru ilikuwa na athari kubwa katika jopo lake.

”Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa, ukweli ni kwamba picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana  unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles