24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

P4R ISAMBAE NCHI NZIMA KUBORESHA SHULE ZA SERIKALI

Na ASHA BANI

ILI wanafunzi waweze kusoma kunahitajika kuwapo mazingira mazuri ya shule na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Pia shule iwe na maabara yenye vifaa vya kutosha ili waweze kujifunza kwa vitendo.

Mazingira mazuri ya shule humfanya mwanafunzi kuweza kupenda shule na hivyo kupunguza idadi ya watoro.

Katika hili, haina budi kuipongeza serikali kwa kuanzisha mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) ulioanzishwa mwa 2014.

Nakumbuka wahenga wana usemi usemao ‘Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, hili ndio naweza kusema kwa baadhi ya mikoa ambayo nilitembelea na kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Programu ya Kitaifa ya Ujifunzaji na Ufundishaji wa Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK) na P4R imefanikiwa kwa kiasi fulani katika mikoa kadhaa.

Miongoni mwa mikoa hiyo ni Mwanza katika Wilaya ya Nyamagana na Ilemela, Ukerewe, Mkoa wa Geita, Singida na Manyara. Ni dhahiri kwamba mafanikio haya yametokana na usimamizi mzuri uliofanywa na wakuu wa shule wakishirikiana na kamati za shule.

Ama kwa hakika majengo yamejengeka, wanafunzi ambao walikuwa wakikaa dawati moja watano, sasa hivi dawati moja linakaliwa na wanafunzi watatu huku kila mmoja akiwa na kitabu chake tofauti na ilivyokuwa awali.

Ikumbukwe kwamba serikali hivi karibuni iligawa vitabu kwa takribani nchi nzima hivyo ni faraja kuona sekta ya elimu imeanza kufanya vizuri.

P4R ilianza mwaka 2014 ambapo imefanikiwa kujenga na kukarabati  miundombinu chakavu ya shule za msingi na sekondari 361 katika halmashauri 129, vyumba vya mdarasa 1,435, mabweni 261, majengo ya utawala 11, mabwalo manne, vyoo 2,832, nyumba za walimu 12, maktaba nne, na uwekaji wa maji katika shule nne.

Pia vyuo vya ualimu 10 vimefanyiwa ukarabati ikiwa ni pamoja na kununua  kompyuta 260 zitakazowawezesha walimu  kutekeleza majukumu yao kwa urahisi. Pia yalinunuliwa magodoro 6,730 kwa ajili ya wanafunzi wa bweni na viti 1976 vya wanachuo.

Aidha, programu imenunua vifaa vya maabara 1,696 kwa ajili ya shule za sekondari kwa ajili ya kufundishia masomo ya Sayansi na kuongeza uelewa kwa wanafunzi.

Sasa basi, ni vema suala hili likafanyika pia katika mikoa ambayo P4R haijafika hasa katika maeneo ya pembezoni mwa mji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles