32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

NYUMBA 100 CHALINZE ZAHARIBIWA NA MVUA

Na Mwandishi Wetu-PWANI

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani Majid Mwanga, amesema nyumba  zaidi ya nyumba 100 zilizopo Kata za Bwilingu eneo la Chalinze Mzee na Msoga zimeharibika na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kutokana na hali hiyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili  kuwasaidia  watu walioathirika na mafuriko ya mvua za masika iliyonyesha juzi.

Mvua hizo zimeathiri baadhi ya maeneo ya Msoga, Chalinze Mzee, darasa moja katika Shule ya Msingi Kidogozero, Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.

Akizungumza na wananchi waliopatwa na athari hizo, baada ya kutembelea maeneo hayo, Mwanga alisema kwa sasa majirani, ndugu wanaendelea kusaidiana.

“Serikali inatafakari cha kufanya kutafuta wadau, ila lazima muhakikishe ndugu zangu mnasaidiana wenyewe kwa wenyewe pasipo kuitegemea Serikali pekee.

“Nashukuru hakuna maafa makubwa makubwa wala ya vifo na majeruhi zaidi ya kubomoka kwa nyumba na kuharibika na sasa tunafanya kila linalowezekana ili kuweza kuwapa msaada wa kibinadamu unatakiwa,” alisema Mwanga

Baadhi ya wakazi waliathirika na mvua hizo akiwemo Rashid Mwinyigoha, alisema mvua hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea  katika eneo hilo na hata kuwasababishia hasara.

Alisema hali yao ni mbaya kwani nguo, fedha, chakula  vimesombwa na maji na sasa hawana la kufanya.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bwilingu, Lucas Rufunga (CCM), alisema wameanza kufanya tathmini ya awali kwa kupita nyumba kwa nyumba ili kubaini hasara waliyoipata wananchi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles