Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM
BEKI wa Simba, Erasto Nyoni, amesema anaamini kila kitu kitakwenda sawa kati yake na Wekundu hao kuhusu mkataba mpya wa kuendelea kubakia Msimbazi.
Mkataba wa miaka miwili wa Nyoni kuichezea Simba unaelekea ukiongoni na kwa sasa kiraka huyo yuko nchini Misri akiwa na kikosi cha Taifa Stars kinachosubiri kushiriki fainali za mataifa ya Afrika(Afcon), ambayo itapigwa nchini humo kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Nyoni alisema mazungumzo kati yake na uongozi wa Simba yanaenda poa, lakini kwa sasa ameelekeza akili yake Afcon, kuhakikisha anaisaidia Stars kufanya vizuri.
“Mkataba wangu utamalizika Julai, kuhusu mazungumzo
ya kuongeza mwingine yanaendelea hakuna
shaka tutaafikiana, acha kwa sasa nielekeze akili Afcon,” alisema Nyoni
ambaye ni zao la kituo cha kuibua vipaji cha Rolling stone cha jijini Arusha.