27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Nyoni awatuliza mashabiki Simba

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BEKI wa Simba, Erasto Nyoni, amesema anaamini kila kitu kitakwenda sawa kati yake na Wekundu hao kuhusu mkataba mpya wa kuendelea kubakia Msimbazi.

Mkataba wa miaka miwili wa Nyoni kuichezea Simba unaelekea  ukiongoni na kwa sasa kiraka huyo yuko nchini Misri akiwa na kikosi cha  Taifa Stars kinachosubiri kushiriki fainali za mataifa ya Afrika(Afcon), ambayo itapigwa  nchini humo kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Nyoni alisema mazungumzo kati yake na uongozi wa Simba yanaenda poa, lakini kwa sasa ameelekeza akili  yake Afcon, kuhakikisha anaisaidia Stars kufanya vizuri.

“Mkataba wangu utamalizika Julai, kuhusu mazungumzo ya kuongeza mwingine yanaendelea hakuna  shaka tutaafikiana, acha kwa sasa nielekeze akili Afcon,” alisema Nyoni ambaye ni zao la kituo cha kuibua vipaji cha Rolling stone cha jijini Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles