26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Nyerere kuendeleza misitu

Na Mwandishi Wetu,Butiama

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), umesema unaendelea kuenzi na kulinda juhudi zote zilizofanywa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake katika kulinda na kuendeleza mazao ya misitu.

Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la maonesho la wakala huo kijijini Butiama mkoani jana, wakati wa maazimisho ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Mwalimu Nyerere, Mkugurenzi wa Idara ya Uzalishaji Mbegu za Miti wa TFS, Dk. Hamza Katety amesema hayati Nyerere alikuwa kiongozi mwenye maoni katika kuendeleza sekta hiyo.

“TFS unaendelea kuenzi kazi nzuri aliyoiasisi Mwalimu Nyerere, wote tunakumbuka sekta ya misitu ilikuwa na mashamba 14, lakini kwa juhudi za huyu mzeek, kwanza aliyaendeleza mashamba yote yaliyoanzishwa na wakoloni, pia akaanza upandaji mkubwa kwenye shamba kubwa kabisa la kutegemewa kama taifa Shamba la Miti la Sao kule Mafinga mkoani Iringa.

“Kama tunavyokumbuka mwanzoni mwa miaka ya sabini kwa wale mnaokumbuka kulikuwa na tatizo kubwa la kidunia la ongezeko la jangwa,Mwalimu alianzisha mkakati mkubwa ya kuondoa ardhi katika Mkoa wa Dodoma iliyokuwa inaitwa HADO yaani hifadhi ardhi Dodoma, na baadae akaupanua mkakati ule mpaka Mkoa wa Shinyanga kuanzisha mkakati huu huu uliojulikana kama HASHI (Hifadhi Ardhi Shinyanga), ni mkakati mkubwa ambao uliacha alama zisizoweza kufutika katika suala zima la uhifadhi na ulindaji wa ardhi,”alisema.

Anasema kwa wale ambao wameshiriki katika matukio ya kuhabarisha umma, wanaweza kutambua mifano na alama ya namna ambavyo Mwalimu alivyoshiriki kusaidia sekta hiyo kwa kuelemisha, kuhabarisha na kushirikisha jamii katika uhifadhi endelevu wa rasilimali za misitu nchi nzima.

“Mwalimu Nyerere amezungumza mambo mengi katika uhifadhi na amesaidia sana kwa hiyo jukumu letu sisi leo tunapomuenzi, moja kama TFS ni kuendeleza ile juhudi ambayo aliiacha…kwa maana hiyo katika mashamba ya miti ambayo yalikuwa 14, sasa hivi tumeongeza hadi kufikia mashamba 24 ambayo mwanzoni yalikuwa na hekta kama 89, lakini sasa hivi tunazo hekta za mashamba ya miti ya kupandwa 185.

“Katika juhudi hizi pia, tumehimiza sana upandaji wa miti kwa jamii, mwaka jana TFS imegawa miche milioni 11 kwa watu binafsi,mashirika na vikundi mbalimbali kwa ajili ya kupanda katika maeneo ya wazi nay ale yaliyohifadhiwa katika mikoa mbalimbali nchi nzima,”amesema.

Amesema sera ya sasa ya TFS ni kuishirikisha jamii katika suala zima la uhifadhi wa misitu na kwa namna hiyo hivi karibuni wamekuwa wakihimiza mno uzalishaji wa mazao ya nyuki katika maeneo mengi ya hifadhi za misitu.

Amesema wananchi wengi wamejihusisha na uzalishaji wa asali kwa sababu ni zao ambalo linawapa thamani ya mapema kutoka kwenye misitu yote iliyohifadhiwa.

Anasema ni shughuli ambayo inafanyika ndani ya hifadhi bila kuathiri hifadhi zenyewe.
“Ndiyo maana tunamuenzi Mwalimu katika siku hii ya leo kwa kukumbuka mchango wake mkubwa katika uhifadhi, utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za misitu,”amesema Dk. Katety.

“Kama mnavyokumbuka Mwalimu huyu huyu ndiye aliyeanzisha shamba la Sao Hili ambalo limekuwa nguzo ya kuzalisha miti kwa ajili ya shughuli mbalimbali,”amesema Dk. Katety

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles