30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bonnah ameamua kukabiliana na changamoto ya taulo za kike shuleni

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, ametoa msaada wa taulo za kike kwa shule 10 za sekondari zilizoko katika jimbo hilo kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo wakati wote.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari Magoza, Bonyokwa, Kinyerezi na Kinyerezi Mpya wakionyesha taulo za kike walizokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa kampeni aliyoianza ya kugawa taulo hizo ambapo ameweka juhudi za kukabiliana na changamoto hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo ambaye yuko bungeni Dodoma, Katibu wake Lutta Rucharaba, amesema msaada uliokabidhiwa leo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Magoza, Kinyerezi, Kinyerezi Mpya na Bonyokwa umetolewa kwa ushirikiano wa Klabu ya Fountain Gate Princess.

Shule nyingine zilizokwishapatiwa msaada huo ni Kiwalani, Ilala, Minazi Mirefu, Majani ya Chai, Kisungu na Ari.

“Mheshimiwa mbunge amedhamiria watoto wa kike wasikose masomo kwa sababu ya taulo za kike, bado shule sita nazo tutazifikia hivyo tunatoa wito kwa wadau wengine mbunge yuko kwenye kampeni muhimu wawiwe kumuunga mkono kusaidia watoto wa kike wasikose masomo,” amesema Rucharaba.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kinyerezi Mpya, Happiness Pallangyo, akipokea taulo za kike kutoka kwa mchezaji wa Klabu ya Fountain Gate Princess, Rose Mpoma. Wapili Kushoto ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Lutta Rucharaba na Katibu wa UWT Kata ya Kinyerezi, Zubeda Chapa.

Naye Ofisa Utawala na Fedha wa Klabu ya Fountain Gate Princess, Happy Joshua, amesema waliona wasiishie kusaidia tu wachezaji wao na kuamua kutanua wigo kwa wanafunzi wa shule mbalimbali na kuahidi kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.

“Tuna wachezaji ambao ni wanafunzi na wamekuwa na changamoto kama hii hivyo tulijaribu kufikiria na wanafunzi wengine,” amesema Happy.

Akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mwajuma Mkuta anayesoma kidato cha pili Shule ya Sekondari Magoza, amesema kukosa vifaa vya kujihifadhi wakati wa hedhi kunaathiri mahudhurio ya wanafunzi hivyo msaada huo utasaidia kukuza kiwango cha taaluma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles