29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Nerandra Modi: Mitandao ya kijamii ilimpa uwaziri mkuu

img4Na Markus Mpangala

LEO katika kitabu chetu tunachosimulia hapa kinaitwa “The Modi Effect: Inside Nerandra Modi ‘s Campaign To Transform India,” kilichoandikwa na Lance Price.

Kimechapishwa na kampuni ya Hodder & Stoughton, Machi 12 mwaka huu. Kimepewa ISBN: 1473610885 ISBN-13: 9781473610880 na kipo katika lugha ya kiingreza.

Lance Price amewahi kuwa mwandishi wa shirika la habati la Uingereza. Kitabu hiki umla ya kurasa 342 kinaelezea hali hali ya uchaguzi mkuu wa India wa mwaka 2014 namna ulivyovunja rekodi mbalimbali.

Madhumuni makubwa ni kuonyesha namna mbinu mpya za kampeni zilizofanywa na timu ya kampeni ya Nerandra Modi pamoja na mwitiko wa wananchi katika suala hilo.

Masimulizi yaliyoko katika kitabu hicho yanalingana na kitabu cha “The Election that Changed India”, kilichoandikwa na Rajdeep Sardesai au kingine cha “Story of Mission272+” kilichoandikwa na Shashi Shekhar.

Kwa upande wake mwandishi Lance Price amewahi kushiriki katika kampeni mbalimbali za kisiasa.  Kati ya mwaka 1998 hadi 2001 alikuwa mshauri wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair pia aliandika kitabu cha  “The Spin Doctor’s Diary (2005). Ikumbukwe ni mwaka 1997 ndipo Tony Blair aliingia madarakani na chama chake cha Labour.

Ndani ya kitabu cha “The Modi Effect: Inside Nerandra Modi’s Campaign To Transform India,”, Lance Price anaelezea hatua kwa hatua namna Modi alivyofanikiwa kuvuna kura nyingi kutoka kwa wananchi.

Price anasema mtu mwenye umri wa miaka 64 ni mzee sana. Katika makuzi yake hakuwahi kutumia mitandao ya kijamii.

Katika umri huo mtu huyo alizaliwa nyakati ambazo mabadiliko ya kiteknolojia bado ilikuwa ya kiwango cha chini. Miaka ambayo wataalamu walikuwa wakihangaika kufanya mapinduzi na ubunifu wa kompyuta.

Nyakati hizo ndiyo alizaliwa Nerandra Modi, waziri mkuu wa sasa wa India. Modi aligombea kupitia chama cha Bharatiya Janata Party (BJP), na alivunja rekodi baada ya kutumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kampeni za uchaguzi huo.

Price anasema, “ushindi huo ulikuwa ni kama kimbunga baharini na rekodi ya kipekee katika uchaguzi wa kidemokrasia nchini India. Ni mshtuko na maajabu mno namna kampeni za kisiasa zilizoendeshwa  kwa miaka mingi bila mbinu mpya. Kampeni za mwaka 2014 zilishuhudia demokrasia ya ajabu ikazaliwa na mwishowe ikampa ushindi  Nerandra Modi na kukiongoza chama chake cha Bharatiya Janata Party(BJP) katika ufahari mkubwa,”

“Si hilo tu, bali asilimia 66.4 (sawa na watu milioni 554) ya wapigakura walikichagua BJP kilichopata ushindi mkubwa tangu kupatikana uhuru wa India. BJP kiliendesha kampeni kisasa kwa kukiangalia kizazi kipya ambacho kimetopea katika matumizi ya mitandao ya kijamii hivyo kikashinda moja kwa moja viti vya Bunge la  Lok Sabha (bunge la chini),”

Maneno yanayoandikwa na Lance Price yanashabiana na maoni yaliyowahi kutolewa na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameroon kuwa ushindi wa Nerandra Modi aliopata Mei 16, 2014 ulikuwa mkubwa mno na hakuwahi kutokea kokote duniani.

Ndani ya kitabu hicho Lance Price anaeleza kinaga ubaga juu ya mbinu za matumizi ya mitandao ya kijamii. Price analinganisha  tofauti ya umri wa Modi na aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Rahul Gandhi.

Anasema, “Nerandra Modi licha ya kuwa na umri wa miaka 64 ikiwa ni 22 zaidi ya mpinzani wake Rahul Gandhi, alifanikiwa kumshinda katika eneo la matumizi ya mitandao ya kijamii, kuvutia idadi wapigakura. Aliuza sera, mikakati, matumaini, alizungumza na wpaigakura, wafuasi wake na wale ambao hawakuwa wameamua kumchagua, na zaidi ubunifu wake mpya wa kuleta maendeleo ya India,”

“Tofauti na alivyokuwa akifikiri Rahul Gandhi kuwa  mitandao ya kijamii haikuwa na manufaa yoyote kwa jamii, lakini kilichotokea alibaini baada ya kumalizika uchaguzi,”.

Anasisitiza kuwa mbinu mpya za mapambano ya kisasa na mikakati ni lazima ihusishe mitandao ya kijamii. Ongezeko la watumiaji limezidi kuifanya mitandao na viongozi mbalimbali kuzungumza na wafuasi wao na wapigakura wapya.

Anasema ili wapigakura wapya wapatikane ni lazima uzungumze nao na kuwapa kitu kipya kitakachofanyika.

Kwamba mgombea au mwanasiasa ni lazima aweke muda wa kutosha na ikibidi wakati mwingine kufuatilia maoni ya wafuasi na wapigaura. Mitandao hiyo itumike kuhamasisha na kuvutia wananchi kwa namna ambayo watamwelewa mgombea wao.

Kwa msingi huo utaona kuwa Lance Price na Nerandra Modi wameingia katika nyakati mpya za kampeni za uchaguzi kwenye mataifa mbalimbali.

Kwamba kitabu hiki kinaweza kutumika kama rejea ili kiweze kuwanufaisha wananchi na wanasiasa kwa ujumla wao.

Hamasa mojawapo iliyowavutia wapigakura ni kitendo cha Nerandra Modi kutokacha mahojiano yoyote aliyokabiliana nayo.

Hali hiyo iliwavutia wapigakura kutaka kumsikiliza zaidi, kumpa nafasi kila mara na washauri wake wa mikakati waliendelea kuhamasisha wananchi wamchague.

Uwezo wa kutoa hotubu nzuri na yenye mvuto ulichangia kupata kura za kuibuka mshindi. Hii ina maana Modi hakukwepa midahalo. Hakutoa visingizio vya kukwepa mahojiano na vyombo vya habari. Aliwafanya wafuasi wake wazidi kusambaza habari zake na kuhamasishana zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles