25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kura ya maoni kuathiri elimu Uingereza?

Wanafunzi nchini UingerezaNa Markus Mpangala

JANA wananchi wa Taifa la Uingereza walishiriki zoezi la kupiga kura kutoa uamuzi wa kuibakisha au kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya. Kura hiyo iliitishwa kufuatia ahadi ya Waziri Mkuu, David Cameron, aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Bila kujali uamuzi uliofanywa jana, lakini kampeni zilipamba moto na kujikuta sekta ya elimu ikiwa moja ya maeneo yaliyoguswa. Maeneo mengine ni ulinzi na usalama wa wanafunzi katika shule zao, pamoja na wananchi wa miji mbalimbali nchini humo.

Iliwagusa wahadhiri, idara na wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu ambao walishiriki zoezi la ama kuibakisha au kuiondoa nchi yao.

Kampeni kubwa inadaiwa kukitikisa Chuo Kikuu cha Cambridge, ambako baadhi ya wanafunzi walisimamishwa masomo sababu ya utovu wa nidhamu.

Miongoni mwa walioendesha kampeni kubwa ni mwandishi wa gazeti la Daily Mail, Katie Hopkins, ambaye aliwatishia wananchi kujali maslahi ya nchi yao hususani sekta ya elimu ambayo inaweza kuathiriwa na matukio ya kigaidi.

Katie Hopkins alisema; “kama kura ya wanaotaka tubaki kwenye Umoja wa Ulaya itashindwa, nawaonya watu wote, msitarajie elimu ya watoto wenu kama itaboreshwa. Nawaonya shule zenu zikishambuliwa msilalamike. Sitaki kuona watu mkija kusema kuna mashambulizi yamefanyika kwa watoto wenu au shule zenu. Wala kusema elimu yenu inavurugwa na mashambulizi kufuatia kukosa usalama. Kwa hiyo nawataka kuwa watu shupavu na kuyakabili hayo yakiwafika.

“Mkiambiwa utafiti wa masuala ya saratani umedorora kutokana na uhaba wa usalama, msije mkalalamika baadaye. Kubalini matokeo ya kazi zenu,” alisema.

Mwanamama huyo alisisitiza kuwa endapo Waingereza watashuhudia vituo vya utafiti wa saratani vinashindwa kufanya kazi basi chanzo ni wao kushindwa kuchukua uamuzi stahiki.

 

EU inadhoofisha elimu ya Uingereza

Licha ya kampeni kubwa inayofanywa na wale wanaotaka kuibakisha Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya, imebainika kuwa taifa hilo linanyonywa.

Ukiangalia sababu za kutaka kujitoa ndizo ambazo zinachangia kudhoofisha mfumo wa elimu ikiwamo utoaji huduma  kwa wanafunzi wa ngazi tofauti.

Uingereza inalipa mchango mkubwa kwenye Jumuiya ya Ulaya kuliko matumizi yake nchini humo.

Kwa mfano; mwaka 2015 Uingereza ilichangia kiasi cha Paundi bilioni 12.9 sawa na wastani wa paundi 200 (Shilingi 600,000) kwa kila Muingereza.

Matumizi ya Jumuiya ya Ulaya nchini Uingereza yalikuwa paundi bilioni 5.8, mchango halisi wa Uingereza ni paundi bilioni 7.1. Wanaotaka kujitoa wanadai fedha hizi zinaweza kutumiwa vizuri kuboresha sekta ya elimu ambayo inakumbana na changamoto mbalimbali nchini humo.

Walikuwa wanapinga Uingereza kuendelea kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya wanaona nchi yao inaathirika na uhamiaji mkubwa kutoka nchi za nje. Mwaka 2015 Uingereza ilipokea wahamiaji zaidi ya 330,000 nusu yao wakitokea nchi za Ulaya Mashariki ambapo baadhi yao wanalazimika kutumia huduma za elimu na kubinya nafasi za wazawa.

Waaliotaka kujitoa waliadai kuwa malipo ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wahamiaji kutoka nchi nyingine za Jumuiya ya Ulaya hasa nchi za Ulaya Mashariki – Poland, Hungary, Slovakia na Jamhuri ya Czech ni mzigo mkubwa.

Pamoja na mambo mengine, hoja kubwa iliyotawala kwenye kampeni hizo ni nafasi ya sekta ya elimu katika umoja wa Ulaya. Wengi waliotaka Uingereza ijitoea wanaamini kuwa wataepuka mashambulizi dhidi ya taifa lao katika shule mbalimbali.

Mathalani vituo vingi vya mapumziko vya wananchi katika miji mbalimbali, pamoja na utekaji nyara wa wanafunzi umekithiri hali ambayo ingeweza kunusuriwa kwa kujitoa kutoka EU.

Pamoja na madai ya sekta ya elimu kunyimwa fedha kutokana na nchi hiyo kutoa michango yake kwenye Jumuiya ya Ulaya, lakini pia inaweza kuiathiri sekta hiyo kwa namna nyingine.

Kitendo cha Uingereza kuwa mwanachama kiliwawezesha raia wake kutumia elimu walizonazo kupata ajira kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.

Utafiti wa taasisi mbalimbali likiwamo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo  (OECD) na vyuo vikuu unaonyesha kuwa Uingereza itaumia kiuchumi na kielimu ikiwa itajiondoa Jumuiya ya Ulaya.

Kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya kutapunguza biashara ya kimataifa, kuwanyima ajira wananchi, uwekezaji kutoka nje na ukuaji wa uchumi. Ikiwa Uingereza itajitoa, biashara ya kimataifa na nchi za Jumuiya ya Ulaya inaweza kupungua kwa asilimia 10 ya pato la taifa na uwekezaji kutoka nje utapungua kwa asilimia 3.4.

Inakadiriwa gharama ya kujitoa kutoka Jumuiya ya Ulaya ni kupunguza pato la Taifa la Uingereza kwa asilimia sita ifikapo mwaka 2030 na kusababisha kila familia ipoteze wastani wa paundi 4300 sawa na Sh milioni 13.7 kila mwaka.

Watu zaidi ya 400,000 wanaweza kupoteza ajira na thamani ya paundi itaporomoka. Aidha, wenye nafasi za kuajiriwa kwenye umoja huo na nchi wanachama wanatajwa kuwa wahanga wakubwa endapo kura ya kujitondoa itawapa ushindi.

Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa mashirika ya habari

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles