Na MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM |
MGANGA Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Festo Dugenge, ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Profesa Hubert kwa kujenga kituo cha kupandikiza mbegu za uzazi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema hatua hiyo inaonyesha namna hospitali hiyo inavyojali afya za wananchi.
Akizungumza katika maadhimisho ya 19 ya kumbukumbu ya mwasisi wa hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake, Dk. Clementina Kairuki, alisema wameamua kujenga kituo hicho ili kusaidia watu wenye matatizo ya kupata uzazi kwa njia ya kawaida, ambao wengi wamekuwa wakienda kupata huduma hizo nje ya nchi.
Alisema baadhi ya wanandoa wanaweza kukaa hata miaka 10 bila kupata mtoto licha ya kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.
“Huenda mmojawapo wa wanandoa anaweza kuwa na tatizo la mbegu zake kuwa hafifu, hivyo watu wa aina hiyo watafika katika …..
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.