30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

CONTE AMGEUZIA KIBAO ABRAMOVICH, ATAKA MAMBO HADHARANI

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa timu ya Chelsea, Antonio Conte, anataka kura ya umma ya kuaminika kutoka kwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich, ili kukomesha hali ya kutokuwa na uhakika wa nafasi yake.

Kocha huyo wa Chelsea ambaye  anakerwa na sera ya usajili ya klabu hiyo, anaelezwa kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake.

Conte ambaye jana usiku kikosi chake kilicheza dhidi ya Watford, amekuwa na presha ya kutemwa na klabu hiyo baada ya mwenendo mbaya wa matokeo ya hivi karibuni.

Abramovich, ambaye yupo jijini London wiki hii, amekuwa na rekodi ya kufukuza makocha watano ndani ya nusu msimu.

Kocha wa Napoli, ­Maurizio Sarri, anahusishwa kuchukua mikoba ya Conte Chelsea.

Conte alisema: “Natakiwa kuwa mkweli, wakati kuna minong’ono kama hii au tuhuma baada ya mchezo wa kwanza wa msimu dhidi ya Burnley, ningependa klabu iandae taarifa rasmi ya kwamba inaniamini katika kazi yangu.

“Lakini kwa kweli nahitaji maelezo ya kupinga tuhuma hizi, changamoto ni kwamba hapakuwa na jambo hili kabla. Ni jambo kubwa kubadili mtazamo uliokuwa sasa, ila kuna mtu mmoja ambaye anaweza kuzungumza na kubadili kila kitu.”

Chelsea iliwahi kutoa taarifa kwa umma Oktoba 2015 ikiwa chini ya Jose Mourinho, ambaye alitimuliwa baada ya miezi miwili wakati huo akiwa ameongeza mkataba wa miaka minne Agosti baada ya kushinda taji la Ligi Kuu England.

Conte  alidai kwamba, anataka kuwa mkweli, kwa kuhitaji mkataba wake usitishwe na kuongeza kwamba: “Tumefanya kazi kubwa katika hii klabu.

“Kama klabu itakuwa imeelewa jambo hili na inataka kuniongezea mkataba mpya, tunaweza kuzungumza.

“Kwanini isiwe hivyo? Matamanio na utayari wangu ni kuendelea kufanya kazi katika klabu hii.”

Conte ameshuhudia Manchester City ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Aymeric Laporte, kuliko wachezaji watatu waliosajiliwa na Chelsea katika usajili wa Januari mwaka huu.

“Kama unajilinganisha na mambo ya nyuma, hali imebadilika sana,” alisema Conte na kuongeza: “Unatakiwa kuelewa hilo baada ya kazi kubwa.

“Nafikiri klabu kama Chelsea inatakiwa kuwa na subira kuliko timu nyingine. “Kujaribu kufanya kazi kwa pamoja na wachezaji unatakiwa kuwa na subira. Msimu uliopita tulifanya jambo kubwa sana, lakini msimu huu hatuko sawa.”

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles