33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

NEC: HATUJAPOKEA MALALAMIKO YA CHADEMA

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM                 |                


SIKU moja baada ya jina la mgombea ubunge wa Chadema katika Jimbo la Korogwe Vijijini, Amina Saguti, kuenguliwa na baadaye chama hicho kudai kuwasilisha malalamiko yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mkurugenzi wa Tume hiyo, Dk. Athumani Kihamia amesema hajapokea barua yoyote ya Chadema.

Juzi, Msimamizi wa Uchasguzi wa Korogwe Vijijini alidai mgombea wa Chadema, Amina alirudisha fomu muda ukiwa umekwisha kupita hali iliyosababisha  mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Timotheo Mzava, kutangazwa kupita bila kupingwa.

Hata hivyo chama hicho kilieleza kuwa mgombea wao alifika katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo tangu saa 5.00 asubuhi lakini barua yake haikupokelewa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dk. Kihamia alisema hajapokea barua yoyote ya malalamiko ya Chadema.

“Hapana hakuna barua yoyote niliyopokea kuhusu malalamiko ya Chadema,”alisema Mkurugenzi huyo wa NEC.

MALALAMIKO YA CHADEMA

Juzi, Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Vincent Mashinji kiliwasilisha barua ya malalamiko NEC, ambayo pamoja na mambo mengine ilimtaka mkurugenzi wa tume hiyo kuitisha mara moja kikao cha maadili cha taifa kwa ajili ya kumjadili msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Korogwe Vijijini.

“Rejea mazungumzo yetu ya simu awali saa 6:03 mchana na ukanirudia saa 06:06 kuhusu msimamizi wa uchaguzi Korogwe Vijijini kutopokea fomu ya mgombea ubunge wa chama chetu ambaye alikuwapo muda wote wa leo (juzi) kuanzia saa 4:00 asubuhi ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jambo ambalo uliahidi kulishughulikia.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles