NA JESSCA NANGAWE
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, amekiri kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa biashara yake imezidi kunawiri na kumwongezea kipato tofauti na alipotoka awali.
Shilole ambaye anamiliki mgahawa maarufu uliopo maeneo ya Kinondoni unaojulikana kama Shish Trump Food, umeendelea kuwa sehemu ya kitega uchumi kwa mwanadada huyo ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na mpenzi wake, Uchebe.
Akizungumza na MTANZANIA, Shilole, alisema amekuwa akipata wateja na oda mbalimbali hali inayoongeza kipato zaidi kwenye biashara hiyo tofauti na alipotoka na kusisitiza huenda hali hiyo imechangiwa na yeye kutulia kwa sasa na kuongeza ubunifu kwenye biashara hiyo.
“Unajua zamani mambo mengi, mara nyingi nilikuwa sishindi hapa, ukweli baada ya kufunga ndoa nimekuwa nikishirikiana bega kwa bega na mume wangu Uchebe, tumekuwa tukibuni vitu zaidi katika kunogesha biashara, kikubwa nashukuru hata mwitikio wa wateja ni mkubwa zaidi,” alisema Shilole.