33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Namba za ushiriki Kili Marathon kutolewa Mlimani City

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waandaaji wa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 zitakazofanyika wiki ijayo mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro wametangaza kituo kitakachotumika kuchukua namba za ushiriki kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotoelwa leo Februari 17, na Kamati ya maandalizi ya mbio hizo za kimataifa, zoezi hilo litafanyika katika sehemu ya kupaki magari katika viwanja vya Mlimani City, karibu na mgahawa wa Pizza Hut siku ya Jumamosi na Jumapili ya wik hii kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

“Tunawaomba waliojisajili mbio ndefu za Kilimanjaro Premium Lager (kilomita 42), mbio za nusu marathon za kilomita 21 za Tigo na zile za kujifurahisha za kilomita 5 za Grant Malt wafike Mlimani City wikiendi hii ili kupewa namba zao za ushiriki tayari kwa mbio hizo mkoani Kilimanjaro tarehe 28 mwezi huu,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mbio hizo, washiriki watahitajika kubeba vitambulisho au hati ya kusafiria wakati wa zoezi hilo lakini pia watahitajika kuonesha ujumbe wa uthibitisho waliopokea wakati wa kufanya malipo. Kwa wale wanaochukua namba za makundi wanatakiwa kubeba nakala za vitambulisho vya washiriki watakaowachukulia na watahudumiwa katika meza ya makundi.

“Tunawaomba wale watakaokwenda kuchukua namba kuzingatia muda kwa sababu zoezi litafanyika kwa siku mbili kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya zoezi hilo kuhamia kwa wakazi wa koa wa Arusha na kufanyika tarehe 23 na 24 mwezi huu katika hoteli ya Kibo Palace na baadae kuhamia Moshi kwa siku tatu kuanzia tarehe 25, 26 na 27 katika hoteli ya Keys,” wamesema waandaaji.

Wameongeza kuwa zoezi la kujiandikisha kwa mbio za kilomita 42 na zile za kilomita 5 kwa ajili ya kujifurahisha linaendelea katika vituo vya kuchukulia namba lakini litafanyika kwa malipo ya papo kwa papo lakini zoezi hilo limefungwa kwa wale wanaotaka kukimbia mbio za kilomita 21.

Wakati huo huo, waandaaji wamesema maandalizi yamekamilika na wanafanya kazi kwa karibu kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine muhimu kama vile Chama Cha Riadha Tanzania (AT) katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kabla, wakati wa mbio na baada ya mbio.

“Tutaweka sehemu za kunawa mikono za kutosha na kutakuwepo na vitakasa mikono (sanitizer) pamoja na kutoa barakoa kwa washiriki katika vituo vya kutolea namba ambazo watatumia kabla ya kuanza mbio kisha watazivua wakati wanakimbia na kukabidhiwa nyingine wakati wanamaliza mbio katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika (MoCU) ili wazivae pale uwanjani,” walisema na kuongeza kuwa kwa washiriki wa mbio za Kilometa 5 watapewa barakoa moja ambayo watatumia kabla ya mbio, watavua wakati wa kukimbia na kuzivaa tena wakati wanaingia uwanjani,” wamesema.

Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager-kwa upande wa mbio ndefu za kilomita 42km, Tigo wamedhamini mbio za kilomita 21km (Half Marathon) wakati Grand Malt wamedhamini mbio za kilomita 5km.

Wadhamini wa vituo vya kunywa maji (water table) ni Unilever Tanzania, Simba Cement, TPC Sugar, Kilimanjaro International Leather Company Limited, Kibo Palace Hotel na watoa huduma maalumu ni Garda World Security, Keys Hotel na CMC Automobile.

Mbio hizi zimeandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kitaifa zinaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions Limited.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles