28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri Mwanga kuweka taa za barabarani kuchochea maendeleo

Na Safina Sarwatt, Mwanga

Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro inatarajiwa kuweka taa za barabarani ambazo zitakuwa zikitumia umeme wa jua hatua ambayo inatajwa kuchochea kwa kasi maendeleo.

Hayo yamebainishwa Februari 16, na Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Tadayo amesema wadau hao wa Maendeleo waishio nje ya Wilaya hiyo wamesema wako tayari kuja kufanya kazi kwa kushirikiana na Madiwani pamoja na wataalam wa halmashauri hiyo ili mji wa Mwanga uweze kukua kwa kasi kimaendeleo.

“Wadau hawa waishio nje ya Mwanga, wamekubali kutusaidia kutuwekea tea za barabarani ambazo zitakuwa zinatumia mwanga wa jua,” amesema Tadayo.

Mbunge huyo amesema tayari wako kwenye mazungumza na Mwekezaji kutoka Kampuni ya DERM ELECTRONIC), ambaye ataweka nguzo hizo na kuwaomba madiwani hao kuridhia mradi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salehe Mkwizu, amesema kukamilika kwa mradi huo wa taa za barabarani utasaidia kuchochea uchumi wa mji wa Mwanga.

“Tunakupongeza sana Mbunge kwa ujumbe wako huo na kwa niaba ya Madiwani wenzangu mradi huu utawasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao hadi nyakati za usiku, put utasaidia kiusalama,”amesema Mkwizu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles