24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa T.I akamatwa na bastola

Z-5-929x1024ATLANTA, MAREKANI

MTOTO wa kike wa rapa T.I, Zonnique Pullins, amekamatwa na polisi baada ya kukutwa na bastola, kwenye uwanja wa ndege wa Jackson International, ikidaiwa alikuwa na lengo la kwenda kukutana na mpenzi wake jijini Atlanta.

Taarifa hizo zimepokelewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wa TI, huku wengi wakimtupia lawama kuwa hamper malezi mazuri mtoto huyo, ingawa yeye amekuwa kimya wala kuonyesha kuguswa na tukio hilo.

Baada ya kuona tuhuma zinazidi kuelekezwa kwake, T.I, aliamua kuwajibu mashabiki hao kuwa haamini kama mwanae anamiliki bastora kama ilivyoripotiwa na askari polisi

“Hayo ni maneno tu ya mashabiki, ninaamini mwanangu  hana bastola, sina wasi wasi na hilo,” alisema T.I.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles