Inspector Haroun kutoa burudani ‘Media Car wash’

InspektaMKONGWE wa rap katuni nchini, Haroun Kihena ‘Inspector Haroun’, leo atatoa burudani ya nguvu kwa wakazi wa Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri katika lile tamasha na Media Car Wash, lenye dhumuni la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanahabari wenye matatizo mbalimbali kiafya.

Akichonga na Swaggaz, Inspector, alisema kuwa amejipanga vya kutosha na kilichobaki ni kutoa burudani kwa mashabiki wake wote watakaojitokeza kwenye viwanja hiyo itakuwa baada ya kuosha magari ya watu mbalimbali.

“ Kesho (leo) tukishirikiana na wabunge na wakazi wa Dodoma tukutane pale Jamhuri, watu walete magari yao tuyaoshe ili tupate fedha za kusaidia wanahabari wenye matatizo kiafya kwa kuwa wana mchango mkubwa kwenye tasnia hii ya burudani, baada ya kuosha magari nitadondosha burudani ya nguvu,” alisema Inspector.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here