23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond kutumbuiza kesho BET kesho

Diamond PlatnumzNYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘’, kesho anatarajia kutoa burudani mbele ya mastaa wa Dunia na wageni mashuhuri kwenye tuzo za Black Entertainment Television (BET), kwenye ukumbi wa Microsoft Theater uliopo Los Angeles, Marekani.

Diamond, ambaye ni msanii pekee anayeiwakilisha Afrika Mashariki, kwenye tuzo hizo akishiriki kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa Afrika ‘Best International Act: Africa’, akichuana na wasanii kama Wizkid, AKA, Cassper Nyovest, Mzvee, Serge Beynoud na Black Koffie.

Hii ni mara yake ya pili kutajwa kwenye tuzo hizo kubwa duniani baada ya mwaka jana kushindwa kuchukua na tuzo kwenda kwa Davido wa Nigeria.

Diamond Platnumz atatumbuiza jukwaa moja na wasanii wakubwa duniani kama Future, Usher Raymond, Bryson Tiller, Alicia Keys na Maxwell endapo wasanii wa Afrika hawatafanyiwa figisu figisu za kupewa tuzo nyuma ya jukwaa kama ilivyokuwa mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles