23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

‘Siri za Familia’ yawaamsha mastaa Bongo

Od YBAADA ya mastaa wa filamu nchini, kuziweka kando tamthilia na kujikita kwenye uandaaji na uchezaji wa filamu kwa kigezo cha maslahi, hivi karibuni wasanii hao wameamka tena nakuanza kuzitolea macho tamthilia mara baada ya tamthilia ya Siri za Familia kufanya mapinduzi makubwa.

Akibonga na Swaggaz, mwongozaji wa tamthilia (DoP) hiyo inayoruka kwenye runinga ya EATV, Edson Suche ‘Od Y’, alisema kuwa wasanii wengi wakubwa wamesahau kuwa tamthilia ndiyo chimbuko la vipaji vya kweli kwa hiyo wamejikuta wapo wenyewe tu na hakuna vipaji vingine vipya vyenye haiba kama yao.

“Tamthilia ina mjenga msanii na ndiyo chimbuko la vipaji vya kweli. Sisi tunafurahi kuona baada ya Siri a familia kuanza kuruka wasanii wakubwa kama kina Jb, Irene Uwoya, Ray na Johari nao wameamua kurudi huku kwenye tamthilia,” alisema Od Y.

Od Y, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, aliongeza kuwa sababu iliyofanya tamthilia hiyo iwashawishi mastaa wakubwa warejee kwenye tamthilia ni ubora na mpangilio mzuri wa hadithi uliofanywa na kampuni ya Jason’s Production waliyoiandaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles