25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

MSAJILI AONYA MATUSI, UCHOCHEZI KAMPENI SIHA, KINONDONI

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amevionya vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha mkoani Kilimanjaro kuepuka fujo, lugha za matusi na uchochezi.

Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Monica Laurent, katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Jaji Mutungi alivitaka vyama vyote vya siasa kutii sheria ya vyama vya siasa, gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchaguzi.

“Natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata. Hivyo natumia fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika chaguzi hizo, kwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kidemokrasia” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha Jaji Mutungi kupitia taarifa hiyo aliwataka wanachama wa vyama hivyo kutoa taarifa katika mamlaka husika pale kitakapo baini kuwapo kwa vitendoi vya uvunjifu wa sheria za uchaguzi badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo katika Jimbo la Kinondoni ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Wananchi  (CUF), Demokrasia Makini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa.

Katika jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro vyama vinavyoshiriki ni CCM, Sauti ya Umma (SAU), CUF na Chadema.

Uchaguzi wa huo ambao kampeni zake zilianza wiki iliyopita huku ikishuhudiwa kuwapo kwa vuta ni kuvute baina ya CCM na Chadema hasa katika Jimbo la Kinondoni unatarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu.

Uchaguzi huo unatokana na wabunge wa majimbo hayo Maulid Mtulia (CUF) kukihama chama chake na kujiunga na CCM kwa madai ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kutokana na kutekeleza mambo mengi ambayo upinzani uliahidi.

Aliyekuwa Mbunge wa Siha, Dk. Godwin Mollel (Chadema), alitangaza kujivua uanachama wa chama chake na kujiunga na CCM kutokana na nia ya dhati ya Serikali ya kutetea rasilimali za Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles