24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mr Blue kuachia ‘Mboga Saba’

BlueNA BEATRICE KAIZA

NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ ambaye hivi karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake, Wayda, amedai anatarajia kuachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Ali Kiba.

Mr Blue amedai kwamba wimbo huo utajulikana kwa jina la ‘Mboga Saba’

Akizungumza na MTANZANIA, Mr Blue alisema kuwa wimbo huo upo tayari na anatarajia kuuachia wiki ijayo endapo mtayarishaji wake, Man Water atamkabidhi.

“Kiukweli huu wimbo haujawahi kutokea na utakuwa bonge la wimbo kwa kuwa tumekutana wakali wa muziki, ninaamini wimbo huo utakuwa ni historia katika tasnia ya muziki hapa nchini,” alisema Mr Blue.

Msanii huyo aliongeza kwa kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa kuupokea wimbo huo wa ‘Mboga Saba’ ambao umefanywa katika studio za Combination Sound, chini ya Man Water.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles