27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Hall: Nitafarijika tukitwaa ubingwa FA

hall-stewart-kocha-wa-azam-fcNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Azam FC, Stewart Hall, amesema wakifanikiwa kunyakua ubingwa wa Kombe la FA itakuwa ni faraja kwake hata kama watashindwa kuchukua ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Azam tayari imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la FA baada ya kuichapa Mwadui FC kwa mikwaju ya penalti 5-3 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Azam sasa inasubiri kuvaana na mshindi atakayepatikana kati ya Yanga na Coastal Union baada ya Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia ripoti ya kamisaa na mwamuzi kutokana na mchezo wao kuvunjika.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Hall alisema kushindwa kufanya vyema katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Esperance ya Tunisia si mwisho wa kikosi hicho, kwani wana uwezo wa kusaka nafasi nyingine ya kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo.

Alisema hafahamu watacheza na timu gani kwenye fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Coastal, lakini malengo yake makubwa ni kuhakikisha wanaibuka na ubingwa.

“Nitafurahi sana kikosi changu kikifanikiwa kuchukua ubingwa wa mashindano yoyote mwaka huu maana hayo ndiyo malengo tuliyojiwekea, tulitolewa Kombe la Shirikisho lakini sasa ndoto zetu mpya ni kutwaa Kombe la FA.

“Bado tunaendelea kupambana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, lakini kinyang’anyiro cha kuwania Kombe la FA ndio tunakabiliana nacho kwa sasa, hivyo ni lazima nianze kupiga hesabu mapema,” alisema Hall.

Kocha huyo raia wa Uingereza, aliongeza kuwa ataendelea kukinoa kikosi kwa kuwapa mbinu mpya wachezaji ili kukiboresha zaidi na kurekebisha makosa ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ili yasijirudie tena.

Timu itakayoibuka bingwa wa FA itapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles