22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Dj JD: Madj tuache unafiki tupendane

jd jdNA FESTO POLEA, MOROGORO

MKALI wa kusugua CD, Dj John Dillinga ‘JD’, ameibuka na kudai kwamba baadhi ya Madj wakongwe hawawapendi wakongwe wenzao wanaoendelea kufanyakazi hiyo hadi sasa.

JD alisema hayo juzi baada ya mashindano makali ya madansa wa zamani wa Mkoa wa Morogoro waliposhindana na wa Dar es Salaam na kutoka suluhu katika ukumbi wa Samaki Samaki mkoani humo.

JD aliyeongozana na Dj Herry, alisema wapo baadhi ya maDJ hawapendi anapojiita ‘legendary’ na wengine hukashifu madjay wenzao waliowazidi uwezo licha ya kuwa na umri mkubwa jambo ambalo linazidi kurudisha nyuma kazi yao hiyo.

“Kuna kipindi nilikuwa kila nikipata nafasi ya kuzungumza jukwaani nilikuwa nikiwakaribisha madj wakongwe ili waje kusema lolote kwa wanaochipukia na kusifia wanaoendeleza fani hiyo, lakini wengi wao walikuwa wakikashifu na kuchukiza fani nzima jambo ambalo halifai na kutokana na hilo naomba madj wote Tanzania tupendane ili kazi yetu ifanikiwe.

“Tunachotakiwa kama mwenzako ana uwezo hata kama mtu mzima na amekuzidi unatakiwa kumpongeza na kumpa heshima yake kwa kuwa wewe huwezi kufanya anavyofanya yeye katika umri alionao,” alieleza na kupongezwa na wengi waliofika katika ukumbi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles