PORTO-NOVO, Benin
MAHAKAMA nchini Benin imemuhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani msomi na mwanasiasa maarufu wa upinzani, Joel Aivo.
Aivo aliyewahi kugombea kiti cha urais, alikuwa chini ya ulinzi tangu Aprili, mwaka huu, na itakumbukwa kuwa alidakwa siku Rais Patrice Talon aliposhinda awamu yake ya pili madarakani.
Mwanasiasa huyo alifunguliwa mashitaka ya uhaini na utakatishaji fedha, ingawa aliyakanusha akisema mahakama imekuwa ikitumiwa na Serikali kuwanyamazisha wapinzani.
Kuhukumiwa kwake kunaendeleza kelele dhidi ya Rais Talon, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kuwanyanyasa wale walioonesha kukosoa mwenendo wa utawala wake.