25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Dini waaswa kutokupotosha umma kuhusu chanjo ya Uviko-19

Renatha Kipaka, Kagera

Viongozi wa dini wametakiwa kuacha tabia ya kuwapotosha wafuasi wao bali waache wao wafanye maamuzi wenyewe katika zoezi zima la kupata chanjo ya Uviko-19 inayoendelea hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji wa Kanisa la Baptist Tanzania, Daniel Mgogo katika emina ya waandishi wa habari na viongozi Mashuhuri iliyoendeshwa kwa njia ya mtandao (Zoom) jana.

“Niseme tu viongozi wa dini tuwe makini na mahubiri tunayotoa kwa jamii sababu janga la Uviko-19 limeunganishwa na mambo mbalimbali ya (66) na (Freemason).

“Hii tabia ya kuwaambia watu wasichanje na wakati umechanja kisirisiri huo nao ni uuwajim”amesema Mgogo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Nickson Simon amesema kuwa, ili kutimiza lengo la kuwafikia watu wengi kuchanjwa itolewe elimu kuanzia ngazi ya jamii.

“Mfano mtu anapomuona jirani yake au mtu anaemfahamu akiwa amechanjwa nirahisi sana kuelewa zaidi zoezi hili la chanjo kuliko mtu mwingine kumueleza,” amesema Simon.

Kwa upande wake Profesa Deodatus Kakoko kutoka Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS) amesema kuwa jamii isione ugonjwa huu kama mzaha kutokana na mila na desturi zilizopo kwa wananchi.

Dk. Kakoko amesema kuwa, ili kuwa na uelewa ni vema watu wasome na kufanya tafiti ili watu waache imani potofu.

Naye mbunge wa Viti maalum, kupitia Asasi za Kiraia, Neema Lugangira amesema serikali kupitia wizara ya afya iendelee kushirikisha viongozi wa kisiasa kuanzia viongozi wa shina ili kutoa elimu sahihi.

Amesema viongozi wamewambia kuwa chanjo ni hiari hivyo kuna mambo ya kuangalia kuwa mtu asipo chanja anakuwa kwenye hatari ya kuugua na kupelekwa chumba cha mahuti ICU lakini pia unapo chanjwa unaepuka kushambulwa na magonjwa hasa inapokuvamia Covid- 19.

“Nitumie nafasi hii kuomba serikali kuwashirikisha viongozi wa dini mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na wasanii ili kutengeneza nguvu ya pamoja”, amesema Lugangira.

Ikumbukwe kuwa mafunzo hayo yamedhaminiwa na shirika la Amref kupitia wizara ya afya hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles