22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yaongeza vifo vya pombe Uingereza

LONDON, England

KWA takwimu za mwaka jana, Uingereza imeshuhudia ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na ulevi wa pombe kwa kipindi chote cha janga la Corona.

Katika hilo, wataalamu wa afya wametaja upweke uliotongana na watu kutakiwa kujitenga ulichagiza wengi wao kujiliwaza kwa pombe.

Takwimu zimeonesha kuwa watu 8,974 walifariki kwa ulevi wa pombe mwaka jana, likiwa ni ongezeko la asilimia 18.6 ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2019.

Ukitazama takwimu hizo, unaona ni ongezeko kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2001, kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles