24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nyumba ya Mchungaji yachomwa moto baada ya maiti kukutwa ndani

LAGOS, Nigeria

VIJANA wenye hasira kali wameichoma moto nyumba ya mchungaji wa kanisa mjini Adebun baada ya mtoto mwenye umri wa miaka saba kukutwa amefariki ndani kwake.

Taarifa zinadai kuwa mtoto wa kike huyo aliyefahamika kwa jina la Demilade, alikuwa amepotea kwa saa kadhaa, kabla ya mwili wake kukutwa ndani ya nyumba ya mtumishi huyo ambaye ni jirani yao.

Kupotea kulikuja baada ya kuagizwa na wazazi wake, ikielezwa kuwa aliingia ndani kwa mchungaji kumfuata mtoto mwenzake ambaye ana tatizo la afya ya akili.

Ulipofanyika msako kwa kushirikiana na majirani, ambapo polisi walishafikishiwa taarifa, ndipo mwili wa Demilade ulipopatikana kwenye nyumba ya mchungaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles