Mo Fire kuachia video mpya

0
509

NA BADI MCHOMOLO

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Mtila Hamisi ‘Mo Fire’, anatarajia kuachia video yake mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Tomorrow’.

Wimbo huo ambao uliandaliwa katika studio za Expendable, video yake imetayarishwa na kampuni ya A, J chini ya Azizi Kikonyo.

“Kwa sasa naanza kwa kuachia video yangu wiki hii na baada ya muda nitaachia wimbo wangu mwingine ili nijitangaze vizuri kimuziki.

“Kuna kazi yangu ipo njiani nimemshirikisha Ney wa Mitego, wimbo huo utaanza kusikika mwakani tumaini langu ni kwamba utakuwa kama wimbo wa Taifa kwa namna utakavyopendwa na kufahamika na kila mtu,” alieleza Mo Fire.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here