Celine arudi kwenye muziki

0
770

celine dionCeline arudi kwenye muziki

LAS VEGAS, MAREKANI

BAADA ya Celine Dion kukaa kwa muda mrefu bila ya kufanya muziki kutokana na kumuuguza mume wake, Rene Angelil, sasa ameanza kazi ya muziki upya.

Celine alipanda jukwaani juzi huku mume wake akiwa pembeni na kabla ya kuimba aliwaambia mashabiki: ‘Nadhani kila mmoja anajua nini ninataka kukufanyia leo siku yangu rasmi.’

Hata hivyo, msanii huyo alijikuta akidondosha chozi kutokana na mapokezi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki wake.

Baada ya kumaliza kuimba msanii huyo aliwashukuru mashabiki hao na kuwaahidi kuwapa burudani mbalimbali siku zijazo.

“Nashukuru kwa uwepo wenu hapa, lakini kikubwa kilichonifanya niwe hapa ni watoto wangu watatu na mume wangu ndio waliniambia nifanye hivi, nawapenda sana watoto wangu pamoja na mume wangu na nipo tayari afie mikononi mwangu,” alisema Celine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here