26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Kongamano la muziki wa reggae kufanyika leo

Innocent Nganyagwa reggaeNA THERESIA GASPER

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House, iliyo chini ya Msanii Mkongwe wa reggae, Innocent Nganyagwa, limeandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini itakayofanyika leo katika makao makuu ya Basata Ilala jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lina lengo la kurudisha muziki wa reggae jukwaani na kujadili mwelekeo wa muziki huo ili urudishe hadi yake.

Ofisa Habari wa Basata, Alistidesi Kwizela, alisema muziki huo haupigi hatua kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hivyo wasanii wakongwe, Innocent Nganyagwa, Innocent Garinoma, Justine Kalikawe na wengineo wameamua kuja na sera za kurudisha hadhi ya muziki huu.

“Nia ya Basata ni kuona wasanii na wadau wote wa muziki nchini wanahudhuria kongamano hilo kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja hatima ya muziki huo, historia yake na namna ya kuburudisha jukwaani na mengine mengi yanayouhusu,” alisema.

Aliongeza kwamba kupitia kongamano hilo muziki huo utakuwa na mwanzo mpya mwema kurudi katika ubora wake.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles