27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA MAGEREZA KUJIELEZA SETHI ASIPOPELEKWA MUHIMBILI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemtaka Mkuu wa Magereza nchini kujieleza endapo mshtakiwa Harbinder Sethi, hatapelekwa kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Uamuzi huo umefikiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi leo, baada ya Wakili wa Sethi, Joseph Makandege kuiomba mahakama leo kufuta kesi hiyo inayomkabili mteja wake na James Rugemarila, ili Sethi apate nafasi ya kutibiwa.

“Naomba mshtakiwa huyo apelekwe Muhimbili na endapo hadi tarehe ya kesi itakapotajwa kama hajapekewa Mkuu wa Magereza aje kujieleza kwa nini hawajampeleka,” amesema Hakimu Shaidi.

Katika maombi yake hayo, Makandege anadai mashtaka hayo yamefunguliwa kwa hila na upande wa Jamhuri umekaidi amri ya mahakama kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Muhimbili, kama mahakama ilivyoamuru zaidi ya mara tatu.

Makandege pia amedai kushindwa kumpeleka hospitali mteja wake kunahatarisha afya yake kwani akikosa kupata matibabu sahihi anaweza kupoteza maisha kutokana na maputo aliyowekewa tumboni.

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwamo ya kutakatisha fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles