Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA
MGANGA wa Tiba asilia, Ashura Mkasanga (33), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma akituhumiwa kumuua Mariamu Saidi (17), mkazi wa Mkoa wa Kigoma kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kisha kukichoma moto.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema mwili wa marehemu ulikutwa kwa mganga huyo katika Kitongoji cha Chang’ombe, Kijiji cha Chamwino Ikulu wilayani Chamwino.
Alisema mwili huo ulikutwa ukiwa umekatwa shingo kwa kutenganishwa na kiwiliwili na kichwa kikiwa kimechomwa moto na kubaki fuvu lisiloweza kutambulika sura yake.
Kamanda huyo alisema baadhi ya sehemu za mwili wa marehemu ambazo ni mkono wa kushoto, shingo, kifua na sehemu za siri ziliunguzwa kwa moto.
“Mnamo tarehe 8 mwezi huu majira ya saa nne usiku katika Kitongoji cha Chang’ombe, Kijiji cha Chamwino Ikulu, mtu mmoja mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mariamu Saidi (17), mkazi wa Kigoma aliuawa kwa kukatwa shingo yake,” alisema.
Kamanda Mambosasa alisema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa mganga huyo asiye na kibali cha kuendesha shughuli za tiba asili, analaza wagonjwa nyumbani kwake, kufanya matambiko na kupiga ramli chonganishi.
Alisema wamewakamata watu 11 wakiwamo wasaidizi wa mganga huyo ambao ni Victor Daniel (24) na mume wa mganga huyo, Noel Mazengo(30)