26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbio za kumtafuta mrithi wa Rais Alassane Outtara zashika kasi

 ABDJAN, IVORY COAST 

VIONGOZI wa chama tawala cha Ivory Coast wamekubaliana kumshinikiza Rais Alassane Outtara kuwania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi wa mwezi Oktoba baada ya kifo cha waziri mkuu Amadou Coulibaly.

Ouattara alitangaza mnamo mwezi Machi kuwa hatowania tena urais baada ya miaka 10 ofisini na tayari alikuwa amemteua Coulibaly kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu.

Muda wa mwisho wa kuwasilisha jina la mgombea wa urais ni Julai 31.

Kifo cha Coulibaly Jumatano wiki hii, ikiwa ni chini ya wiki moja tangu aliporejea kutoka mapumziko ya kimatatibu nchini Ufaransa, kutokana na matatizo ya moyo, kimekiacha chama tawala cha RHDP kikihaha kupata mgombea mwingine.

Uchaguzi huo wa Oktoba unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa tangu mwaka 2010 baada ya ushindi wa Ouattara dhidi ya Laurent Gbagbo, ushindi uliochochea vita vilivyosababisha vifo vya watu 3,000.

Coulibaly, alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Alkhamisi akiwa na umri wa miaka 61.

Waziri Mkuu Coulibaly alishiriki kwenye kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri la serikali ya Kodivaa, hali yake ikawa mbaya na alifariki dunia hospitalini.

 Mwezi Machi mwaka huu, Coulibaly aliteuliwa na chama tawala wa Ivory Coast kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho ili kumrithi Rais Alassane Ouattara.

Waziri Mkuu huyo alirejea nchini Kodivaa Julai 2 mwaka huu baada ya kupitisha muda mrefu wa matibabu nchini Ufaransa. 

Aliwahi kufanyiwa operesheni ya moyo mwaka 2012.

Ouattara amemtaja Colibaly kwamba alikuwa mtu wake wake wa karibu mno katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. 

Haikuweza kujulikana haraka ni nani atateuliwa kushika nafasi yake ya kugombea urais wa tiketi ya chama tawala katika nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa cocoa duniani.

Hamed Bakayoko ndiye aliyesimamia ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa muda wa miezi mwili. 

Uchaguzi ujao nchini Ivory Coast unahesabiwa kuwa ni mtihani wa kupima utulivu na amani katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika yenye historia ya machafuko ya uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles