27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbwa wafukua makaburi ya watoto zaidi ya 300 Msumbiji

 MAPUTO, MSUMBIJI 

MBWA wanaozurura mitaani (pichani) nchini Msumbiji wamekua wakifukua makaburi mengi ya watoto katika makaburi ya mji wa Chimoio.

Wakaazi wa mji huo wamekiambia kituo cha runinga cha Miramar.

Mama mmoja amesema siku chache zilizopita baada ya kumzika mwanawe, alienda makaburini kufanya usafi lakini alipofika hapo alikuta mbwa tayari wamefukua na kula maiti ya marehemu mwanawe.

Ripoti za vyombo vya habari nchi humo zinaonesha vipande vya nguo na mifupa na nyama ya binadamu iliotapakaa katika eneo la makaburi ya umma.

Mwandishi wa kituo cha runinga cha Miramar ameiambia BBC kwamba katika kipindi cha wiki tatu makaburi 343 ya watoto yalifukuliwa na mbwa hao wa mitaani.

Wakaazi wanasema mbwa hao wamekuwa tatizo la kila siku na kwamba hali imekuwa mbaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni kwa sababu ni watu wachache wanaoruhusiwa kufika katika maziko hayo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Janga la virusi vya corona pia limewafanya watu kupoteza kazi na huenda hawana uwezo wa kukimu familia zao wala kuwalisha wanyama wao.

Hatua ya makaburi ya umma kutozungushiwa au imesemekana kuchangia tatizo hilo.

Wenyeji wanasema

Mamlaka ya mji wa Chimoio, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Manica karibu na mpaka wa Zimbabwe, haikuwepo kutoa tamko kuhusiana na hali hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles