25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi ya Corona nchini Iran yapindukia 250,458

 TEHRAN, IRAN

WIZARA ya afya nchini Iran imesema idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo imepindukia 250,458. 

Wizara hiyo imeongeza kuwa watu 221 wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa mapafu katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya watu waliofariki nchini humo kuwa 12,305.

Iran ni miongoni mwa nchi zilizoathirika pakubwa na janga la Covid-19 katika kanda ya Mashariki ya kati.

Jumamosi iliyopita, Rais Hassan Rouhani alitangaza hatua mpya za kukabiliana na kuenea kwa virusi hivyo, na kuonya kuwa raia wa Iran wasiovaa barakoa watanyimwa huduma za serikali.

Kiongozi wa juu kabisa nchini humo Ayatollah Ali Khamenei ameonekana katika runinga ya kitaifa akiwa amevaa barakoa katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema litachunguza jinsi ilivyoshughulikia janga la Corona

WHO lilitangaza juzi kuwa linaunda jopo huru ili kuchunguza jinsi lilivyoshughulikia janga la Covid-19.

 Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameuambia mkutano wa wawakilishi 194 wa WHO uliofanyika kwa njia ya mtandao, kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand Helen Clark na aliyekuwa rais wa Liberia Ellen Johnson Sirlef wamekubali kuongoza jopo hilo na pia kuchagua wanachama wake.

Tedros amesema kuwa huu ni wakati wa kutafakari na kuyaelezea mataifa wanachama wa shirika hilo kuwa walikubaliana kwa kauli moja mnamo mwezi Mei kutathmini jinsi shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilivyoshughulikia janga la virusi vya Corona. 

Utawala wa rais Donald Trump wa nchini Marekani, umelikosoa shirika hilo kwa namna lilivyoshughulikia janga hilo, na wiki hii umemuandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kumuarifu juu ya uamuzi wake kujitoa katika shirika hilo mwaka ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles